Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanafunzi kidato cha kwanza adaiwa kupewa ujauzito na babu miaka 65

Mimba Mashuleniiii Mwanafunzi kidato cha kwanza adaiwa kupewa ujauzito na babu miaka 65

Thu, 6 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga linamsaka Mzee Amos Samsoni (65) Mkazi wa Kijiji cha Mwamala Kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga, ambaye amekimbia kusikojulikana akituhumiwa kumpatia ujauzito Mwanafunzi wa Kidato cha kwanza (16) katika Shule ya Sekondari Kolandoto (jina limehifadhiwa) na kumkatisha masomo yake.

Kamanda Magomi amebainisha hayo wakati akiongea na waandishi wa habari, kwamba ni kweli kuna tukio la Mwanafunzi kudaiwa kupewa ujauzito na Mzee huyo ambaye kwa sasa wanamsaka mara baada ya kukimbia kusikojulikana.

“Jeshi la Polisi tunamtafuta mtuhumiwa ambaye amedaiwa kumpatia ujauzito Mwanafunzi sababu alitoroka kabla hajamkamatwa,”alisema Magomi.

Mwanafunzi huyo akielezea namna alivyoingia kwenye mahusiano ya kimapenzi na Mzee huyo, amesema alimuita nyumbani kwake na kumpatia kiasi cha fedha Sh.2,000 na siku nyingine tena alimpatia Sh.5,000 kisha akamlazimisha kufanya naye mapenzi.

Alisema baada ya hapo waliendelea kuwa wapenzi hadi akashika ujauzito, lakini baadae alichukizwa na kitendo cha Mzee huyo kumtaka tena ndugu yake kimapenzi ndipo wakaendea kutoa taarifa katika familia kuwa amepewa ujauzito na mzee Amosi Samsoni ambaye ni katibu katika uongozi wa kijiji.

Aidha, alisema baada ya kikao cha familia kukaa kujadili jambo hilo, walikubaliana mzee huyo atoe faini ya magunia mawili ya mpunga na Baiskeli ili kumaliza suala hilo, huku yeye akiacha masomo na kubaki kulea ujauzito ambao kwa sasa una miezi mitano.

Baada ya kikao hicho cha familia, baadhi ya wanawake katika kijiji hicho hawa kukubaliana na jambo hilo wakidai mzee huyo amekuwa na tabia ya kurubuni wanafunzi na kufanya nao mapenzi na kuwaharibia maisha yao, ndipo wakatoa taarifa kwa Jeshi la Polisi ili akamatwe na sasa amekimbia kusikojulikana.

Nao wadau wa kupinga vitendo vya ukatili mkoani Shinyanga wakiwamo (SMAUJATA), wameliomba Jeshi la Polisi mkoani humo kuhakikisha wanamkamata mzee huyo na kuchukuliwa hatua kali za kisheria ili liwefundisho kwa watu wengine.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: