Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwamba apambana na mamba kwa dakika 15 Lindi

Mamba Mwamba apambana na mamba kwa dakika 15 Lindi

Thu, 30 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkazi wa Kata ya Rutamba, Manispaa ya Lindi, Salum Kindamba (44), amelazwa Hospitali ya Rufani Sokoine mkoani Lindi baada ya kushambuliwa na mamba wakati akivua samaki na wenzake katika eneo la Bwawa la Katani, Kata ya Rutamba.

Tukio hilo lilitokea Machi 11, mwaka huu, majira ya saa 9:00 usiku wakati Kindamba na wavuvi wenzake wakiwa wanavua samaki.

Akisimulia mkasa huo hospitalini hapo, Kindamba alisema akiwa na wavuvi wenzake waliondoka nyumbani majira ya jioni ili wakavue samaki kwa ajili ya kujipatia kipato na kitowewo.

Kindamba ambaye amejeruhiwa na mamba huyo maeneo ya kifuani, bega la kushoto, tumbo na kushonwa nyuzi, usoni, shavuni na kidevuni, alisema akiwa anatega nyavu ndani ya bwawa hilo, mamba aliyekuwa mawindoni alimvamia na kumng’ata mkono wa kushoto eneo la bega.

Alisema wakati mamba akijaribu kumvuta kwenye maji ya kina kirefu, alijihaki kwa kutumia mkono wake wa kulia kumpiga mamba ngumi ya kichwa na kumwachia kisha kuondoka zake, hata hivyo, alisema alirejea tena na kumng’ata sehemu zingine za mwili wake, hali iliyomfanya atumie mkono wake mwingine kumpiga ngumi kwenye pua.

Aliendelea kusimulia kuwa baada ya ngumi hiyo alimwachia, lakini alimrudia tena na kumng’ata mikono yote miwili na kujaribu kumvuta kwenye maji yenye kina kirefu, ndipo mvuvi huyo alipojihami kwa kutumia kichwa chake kumpiga mamba huyo, ambaye hatimaye alimwachia na kuondoka zake.

“Ilinichukua dakika 45 kuanzia saa 9:05 usiku hadi 9:55 naendelea kupambana na mamba aliyekuwa amenivamia,” alisema Kindamba.

Alisema baada ya mamba huyo kumwachia, wavuvi wenzie walimfuata na kumpakia kwenye mtumbwi waliokuwa wanavulia samaki na kumkimbiza Kituo cha Afya Rutamba kwa ajili ya matibabu na baadaye kuhamishiwa hospitalini humo.

Mganga Mfawidhi Hospitali ya Sokoine, Dk. Godwin Macheku, alithibitisha kumpokea mvuvi huyo akiwa katika hali mbaya, lakini baada ya matibabu alisema anaendelea vizuri.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: