Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muuguzi KCMC Moshi auawa kikatili

MUUGUZII Khudheifa Changa

Thu, 6 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro linawashikilia watu watano kwa tuhuma za mauaji ya Khudheifa Changa (26), ambaye alikuwa ni Muuguzi wa Hospitali ya Rufaa ya KCMC Moshi, Kilimanjaro.

Inadaiwa Khudheifa Changa aliuawa usiku wa kuamkia Julai 2, mwaka huu wakati akipita katika uchochoro wa Mtaa wa Marindi mjini Moshi, katika purukushani alijeruhiwa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali kwenye mbavu ya kushoto usawa wa moyo.

"Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na raia wema lilifanikiwa kupata taarifa zilizosaidia kukamatwa kwa watuhumiwa watano ambao walitoweka baada ya kutenda unyama huo, na watafikishwa mahakamani upelelezi utakapokamilika," amesema ACP Maigwa.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ACP Simon Maigwa, amesema kuwa watuhumiwa hao ambao watatu ni wanaume na wanawake wawili walikuwa na nia ya kumpora mali alizonazo, na kwamba watafikishwa mahakamani upelelezi utakapokamilika.

Kwa upande wake Afisa Uhusiano wa Hospitali ya Rufaa ya KCMC Gabriel Chisseo amesema marehemu alianza kazi Februari Mosi mwaka huu akiwa amekaa kazini kwa miezi minne hadi umauti ulipomkuta.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: