Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto apigwa radi akicheza na wenzake

Radi Yaua Wachezaji Wa Soka Magharibi Mwa Kenya Mtoto apigwa radi akicheza na wenzake

Tue, 14 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Swaumu Abdala (13) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya msingi Bugongwa mtaa wa Igombe B kata ya Bugogwa halmashauri ya manispaa ya Ilemela amepoteza maisha baada ya kupigwa na radi wakati akikinga maji na kucheza kwenye mvua na wenzake jirani na nyumbani kwao.

Ndugu wa mtoto huyo wamesema wakati tukio hilo likitokea marehemu na wenzake walikuwa wakichota maji na kucheza kwenye mvua ndipo mtoto huyo mmoja alipo pigwa radi.

Mganga mfawidhi wa kituo cha afya cha Karume Dk Thomas Shija akithibitisha kutokea kwa kifo hicho amesema walimpokea mtoto huyo siku ya jumamosi majira ya saa tano akiwa amefariki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: