Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mnyama wa ajabu azua taharuki

Mnyama Komba Mnyama aina ya Komba

Mon, 26 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya baadhi ya Wananchi wa Kitongoji cha Chamamba maarufu kama 'Sumbawanga ndogo' Mkoani Iringa kupata taharuki baada ya kudai kumuua Mnyama wa ajabu, Mtaalam wa Wanyama pori amesema kuwa Mnyama huyo sio wa ajabu bali kilichotokea ni Wananchi hao kushindwa kumtambua.

Mtaalamu huyo baada ya kutazama picha zilizosambaa mtandaoni amesema Mnyama huyo ni Komba (Bush Baby) na kwamba Tanzania inao Komba wakubwa na wadogo ambapo hujulikana pia kama Watoto wa msituni (Bushbabies/Galagos) wakiwa ni Wanyama wadogo wenye asili ya nyani (primate) katika kundi la mamalia (wanaozaliana) na huonekana zaidi usiku( nocturnal) wanapokuwa wanakula na vilevile uwezo wao wa kuona mchana ni mdogo ndio maana ni nadra kuwaona mchana.

Mapema leo Wananchi wa Kijiji cha Mkombilenga walichukua maamuzi ya kumuua Mnyama huyo kwa imani kuwa anatumika kishirikina baada ya kugundua kuwa ana sauti kama ya Mtoto mchanga na sehemu zake za siri ni kama za Binadamu Mwanaume.

Mwenyekiti wa Kijiji hicho amesema kuwa walikiona kiumbe hicho juu ya mti na walipoulizana hata na Wazee wa Kijiji walishindwa kumfahamu kwakuwa ana mikono kama Binadamu na amechanjwa masikioni.

Mtaalamu wa Wanyamapori amesema; "Komba wana macho makubwa na mikono yenye vidole kama Binadamu sawa na aina nyingine ya nyani, jina la Bushbaby lilitokana na Wanyama hawa kulia kama Watoto na kama unakaa maeneo yenye miti mingi usiku utawasikia na unaweza kuhisi kuna Mtoto analia msituni."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: