Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkandarasi apasua Bomba la mafuta (TAZAMA) Mbeya

Bomba La Mafuta TANGA Mkandarasi apasua Bomba la mafuta (TAZAMA) Mbeya

Fri, 26 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bomba la Mafuta la Tanzania na Zambia (TAZAMA), limepasuka katika eneo la Swaya, Jijini Mbeya na kusababisha kiwango kikubwa cha mafuta, kuvuja na kusambaa mitaani hali ambayo imezua taharuki kwa wananchi wanaoishi katika eneo hilo.

Hayo yamesababishwa baada ya mkandarasi anayejenga barabara kulikata na greda wakati akijenga katika kijiji eneo hilo.

“Wakati tunafanya finishing kwenye approaching road za daraja, injinia na operator wa greda walikuja kipande hiki, baada ya muda mfupi wakanipigia simu kwamba wamekata bomba la mafuta, nikaja eneo la tukio na kuanza kutafuta mamlaka husika kwa maana ya TAZAMA na vyombo vyote vinavyohusika,” amesema msimamizi wa mradi huo.

“Kuna kazi ya heavy reshaping waliokuwa wakifanya, upande mmoja alifanya kilomita 1.5 na upande wa pili kilomita 1, wakati wakifanya hapa walijua kabisa kuna bomba la mafuta kwa hiyo ni sehemu ya kuruka, sasa sijajua alifanyaje akajichanganya akakata bomba,” amesema DC wa wilaya hiyo.

Baada ya kukata bomba, mafuta hayo yalianza kutitirika kuelekea mto Nzove na kuzua taharuki kwa wananchi wa eneo hilo.

“Nilikuwa nimekaa klabuni nikaona kama maji, nilipofuata yale maji ndipo nikakuta kumbe ni mafuta yanatiririka baada ya bomba kukatwa na greda. Nilidhani ni shoti au trekta limeungua, mafuta yalikuwa yakiruka juu,” amesema mwanakijiji.

“Tulichokifanya ni kuimarisha ulinzi na kushirikiana na meneja wa TAZAMA, hali hii imeshaonekana kwa kiwango hiki, niwaombe wananchi wote wa eneo hili wachukue hatua ya maksudi kuhakikisha kwamba upotevu wa mafuta haya hautokei tena,” amesema ofisa wa polisi aliyefika kuhakikisha usalama eneo hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: