Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miili ya wanaume watano yaokotwa

Maiti Miili ya wanaume watano yaokotwa

Thu, 11 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zoezi la kumtambua miili ya watu watano (5) iliyookotwa ikiwa imetupwa kando ya barabara ya lami eneo la Mlima Senjele, Kata ya Nanyara, wilayani Mbozi; Mkoa wa Songwe, linaendelea.

Hata hivyo, muda ambao waandishi anaandika habari hii, hakukuwa na mwili hata mmoja uliotambuliwa na ndugu, jamaa ama marafiki.

Tukio la kuonekana kwa miili ya watu hao ambao inasemekana ni wa jinsia ya kiume wakikadiliwa kuwa na umri wa kati ya miaka 25 na 30; limetokea jana ambapo walioiona miili hiyo jana Mei 10 ,2023 walisema ilikuwa ikivuja damu kichwani.

Wakati akiongea kwa njia ya simu na mwandishi wetu juu ya zoezi hilo la utambuzi wa miili hiyo iliyookotwa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Kamishna Msaidizi wa Polisi Theopista Mallya; amesema bado miili hiyo haijatambuliwa.

Hata hivyo Kamanda huyo amesema, tayari Jeshi la Polisi limetoa taarifa kwa jamii na hasa wale ambao wamepotelewa na ndugu zao wanaokadiliwa kuwa na miaka 25 mpaka 30, kufika hospitali ya wilaya (Vwawa) kwa ajili ya kuwatambua marehemu hao.

“Mpaka sasa hakuna mwili ambao umetambuliwa pamoja na baadhi ya watu kufika hospitalini kwa ajili ya kutambua miili ya marehemu, niwakumbushe ndugu ambao hawajawaona vijana wao siku za hivi karibuni kufika katika hospitali ya wilaya kwa ajili ya utambuzi,” amesema Kamanda Mallya.

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Mbozi, Dk Keneth Lesilwa amesema Mei, 10 mwaka huu saa saba mchana, polisi waliwapelekea miili mitano ya jinsia ya kiume.

Kwa mujibu wa mganga huyo, marehemu hao hawana majeraha makubwa sana isipokuwa wameonekana kuwa na michubuko sehemu za usoni na kuvimba vichwa, huku akidai kuwa uchunguzi zaidi unaendelea ili ndugu waweze kuwatambua marehemu hao.

“Mpaka sasa ni watu wachache wamefika hospitalini kwa ajili ya utambuzi lakini hakuna aliyetambulika. Nawashauri ndugu na jamaa wafike hospitali kuwatambua marehemu, kabla utaratibu mwingine wa halmashauri haujachukuliwa ikiwa watakaa hospitalini hapo kwa muda wa zaidi ya wiki moja,” amesema Dk Lesilwa.

Mmoja wa watu waliofika kumtambua miili hiyo Juma Mwakateba mkazi wa Mlowo, ambaye kimsingi alilazimika kufika hospitalini hapo kutokana na mtoto wake kuondoka hivi karibuni bila kuaga wala kuacha mawasiliano yoyote.

Hata hivyo akiwa na Furaha iliyochanganyika na huzuni, Mwakateba anabainisha kuwa, hajauona amesema hajauona mwili wa mwanaye, hata hivyo; analaani mauaji hayo ambayo yanasadikika kutokea usiku wa kuamkia Mei, 10 mwaka huu na kutupwa katika milima ya Senjele.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: