Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbongo, Mrundi jela kwa kuvunja ofisi na kuiba pikipiki ya mganga mkuu

Jela 1.jpeg Mbongo, Mrundi jela kwa kuvunja ofisi na kuiba pikipiki ya mganga mkuu

Tue, 19 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu wawili akiwemo raia wa Burundi, Niyokindi Anthony (44), wamehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka sita jela baada ya kukiri kutenda kosa la kuvunja Ofisi ya Mganga Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza na kuiba pikipiki tatu zenye thamani ya Shilingi Milioni 11, 850,000.

Akiwasomea maelezo ya kosa washtakiwa, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Sajenti wa Polisi Theophilius Bei amesema washtakiwa walitenda makosa hayo Agosti 20,2023, kwa kuiba pikipiki tatu za Serikali zenye namba ya usajili, SM15342, SM15343 na SM15349, zote aina ya Yamaha kinyume na Kanuni ya adhabu Sura ya 16 toleo la mwaka 2022.

Mshtakiwa mwingine aliyehukumiwa kutumikia kifungo hicho, ni Ibrahim Mshengezi (55), mkazi wa Isungangh’olo Wilayani Sengerema, ambapo wamehukumiwa kwa kutenda makosa mawili ya kuvunja Ofisi na kuiba kinyume na vifungu 297 na 258 vya Kanuni ya Adhabu sura ya 16, iliyofanyiwa marejeo mwaka 2022.

Katika kesi hiyo yenye washtakiwa watatu, mshtakiwa mmoja Mkazi wa Isungangh’olo wilayani Sengerema, Anold Paul (25), alikana mashtaka hayo ambapo Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo, Evod Kisoka ameamuru arejeshwe rumande baada ya kukosa wadhamini.

Hata hivyo, shitaka dhidi ya mshitakiwa namba tatu Anold Paul, ambaye amekana mashtaka hayo litaendelea Oktoba 10, 2023 huku Hakimu Kisoka akisema Mahakama imetoa hukumu hiyo ya miaka sita kwa washtakiwa, ili iwe funzo kwa wengine wenye tabia kama hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: