Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mazito yaibuka wapenzi waliokutwa wamefariki, mama asimulia!

Rachel Izengo Pic Rachel Izengo.

Tue, 19 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mama mzazi wa marehemu Esther, Rachel Izengo amesema jina la mtoto wake ni Esther Ramadhani Isugilo na siyo Samira Mathias ambalo lilizoeleka mtaani.

Esther amefariki dunia usiku wa kuamkia jana Jumatatu Septemba 18, 2023 kwa madai ya kuchinjwa na mpenzi wake aliyefahamika kwa jina moja la Amos.

Mapema leo asubuhi mmliki wa nyumba aliyokuwa amepanga Esther ambako kulifanyika mauaji hayo, Yohana Nhembelo alisema ndugu wameomba chumba kilichofanyika kisifanyiwe usafi hadi watakapofika na kukiangalia.

Amesema amepata taarifa ya kifo cha mtoto wake kupitia kwa majirani saa 10.00 usiku wa kuamkia leo akiwa mkoani Shinyanga ambako ndiko anakoishi.

Amesema alianza safari muda huo na kufika jijini Dodoma saa 8:00 leo ili kujua sababu ya kifo cha binti yake ambaye ni mtoto wa kwanza kati ya watoto watatu alionao.

“Nimesikitishwa sana na kifo cha mwanangu cha kuchinjwa kwa sababu ni kifungua mimba na sikutarajia kama atakufa kwa kifo kama hiki. Binti yangu alikuwa ni mtu wa watu,”amesema huku akiangua kilio baada ya kushuhudia chumba kichofanyika mauaji hayo.

Ndugu wa marehemu wamesema baada ya kuangalia hali ya mwili wa mtoto wao ndipo watafanya uamuzi wazike wapi.

Rachel amesema anatamani kama ataweza kuondoka na mwili wa binti yake kwenda kumzika mkoani Shinyanga kwasababu hawezi kumzika mwanaye kwenye mji wa ugeni (Dodoma).

Babu wa Marehemu yake Esther, Daudi Lazaro amesema ni mapema kuzungumzia taratibu za mazishi kwa sababu wameondoka ghafla bila kuwashirikisha ndugu wengine lakini baada ya kuwasiliana nao watajua watazika wapi.

Amesema uamuzi wa kumzika Dodoma au kusafirisha utafikiwa baada ya kuona hali ya mwili ulivyo na kuwataka ndugu pamoja na majirani kuvuta subira wakati wakifanya maamuzi ya wapi pa kumzika.

Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, Martin Otieno amesema kuwa chanzo cha mauaji ya wapenzi hao waliokutwa wamefariki dunia usiku wa kuamkia ni wivu wa mapenzi.

Kamanda huyo amesema mwanaume aliyejulikana kwa jina moja la Amos alimchoma kisu maeneo ya shingoni Esther maeneo ya shingoni kama mara tatu na kupelekea koromeo kutoka nje na akawa amemchoma kwenye mkono begani kisha yeye kujichoma kisu kwenye kitovu na kupelekea utumbo wote kutoka nje.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: