Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mauaji tena! Mume amuua mkewe kwa kuchelewa kwenye harusi

Mauaji Mara  Mauaji tena! Mume amuua mkewe kwa kuchelewa kwenye harusi

Mon, 30 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi Wilaya ya Serengeti mkoani Mara inamshikilia Werema Marwa (46) mkazi wa Kijiji cha Tamkeri Kata ya Mbalibali kwa tuhuma za mauaji ya mkewe, Pili Mgaya (24) chanzo kikiwa ni wivu wa mapenzi baada ya kuchelewa kutoka kwenye harusi.

Tukio hilo linadaiwa kutokea Mei 26 mwaka huu majira ya saa 6:00 usiku baada ya Pili kurejea nyumbani akitokea kwenye harusi Kijiji cha Nyamburi hadi Tamkeri ambapo mumewe huyo alianza kumpiga na kumchoma kwa kitu chenye ncha kali kilichomsababishia umati kwa madai kwamba ana mwanaume mwingine.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara, Longinus Tibishubwamu amekiri kutokea kwa tukio hilo na mtuhumiwa alikamatwa akijaribu kutoroka kuingia ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia lango la Tabora B.

Kamanda huyo anasema, jalada la mtuhumiwa limefikishwa ofisi ya Mashtaka Wilaya kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: