Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mama anusurika kifo baada ya kupigwa na sungusungu

Mama Motoooooo Mama anusurika kifo baada ya kupigwa na sungusungu

Mon, 17 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Manka Mushi mwenye miaka 26 mkazi wa Ikoma, Kata ya Itilima wilayani Kishapu mkoani Shinyanga amenusurika kifo baada ya kupigwa na Jeshi la Jadi Sungusungu kwa tuhuma za wizi wa 420,000.

Akizungumza na Azam News katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga alipolazwa akipatiwa matibabu Manka amesema tukio hilo lilimsibu usiku wa Aprili 14 baada ya mwanaume aliyekuwa akimtaka kimapenzi kumkataa na kuamua kusema kuwa amemuibia pesa hizo.

Amesema baada ya tukio hilo mwanaume huyo alimshika kwa nguvu na kumtishia kumuua kwa kumnyonga shingo hadi akajisaidia haja kubwa kisha kumfikisha kwa sungusungu ili aadhibiwe ambapo aliadhibiwa viboko vilivyochangia kupoteza fahamu.

Kwa upande wake, Afisa Ustawi wa Jamii Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga, Prisila Mushi amesema mtu huyo alipokelewa Aprili 14 akiwa na hali mbaya na baada ya matibabu anaendelea vema huku akiwa amejeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili hususani makalio na mgongoni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: