Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mama adaiwa kumnyonga mwanaye wa kumzaa

Crime Scene 45.jpeg Mama adaiwa kumnyonga mwanaye wa kumzaa

Thu, 2 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya, linamshikilia Regina Issack (40), anayedaiwa kuwa na matatizo ya akili, mkazi wa Ilindi, Kata ya Ilemi jijini Mbeya kwa tuhuma za mauaji ya mtoto wake, Sisela Ngailo (09).

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP, Benjamin Kuzaga amesema tukio hilo limetokea Februari 23, 2023 majira ya saa 7:00 mchana ambapo Regina alimnyonga  shingo mwanae akiwa amelala.

"Chanzo cha tukio hili inasadikika mtuhumiwa kuwa na tatizo la afya ya akili ambapo alikuwa akihudhuria  matibabu ya afya katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya (MZRH) tayari uchunguzi wa tukio hili unaendelea na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika," amesema Kamanda Kuzaga. 

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: