Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kigoma: Miili ya wanafunzi wote waliozama mtoni yapatikana

Zabibu Jumanne Miili ya wanafunzi wote waliozama mtoni yapatikana

Thu, 2 Mar 2023 Chanzo: Mwananchi

Mwili wa mwanafunzi Zabibu Jumanne (8) ambaye ndiye pekee alikuwa hajapatikana kati ya wanafunzi wanne wa Shule ya Msingi Kagera Manispaa ya Kigoma Ujiji waliozama ndani ya maji ya Mto Luiche baada ya mtumbwi waliopanda kupinduka umepatikana.

Kupatikana kwa mwili wa Zabibu kumefanya idadi ya miili iliyopatikana tangu mtumbwi huo upinduke Februari 24, mwaka huu kufikia nne, na hivyo kuhitimisha kazi ya uokoaji iliyodumu kwa siku sita tangu mtumbwi wao ulipozama Ijumaa ya Februari 24, 2023.

Miili ya wanafunzi wawili, Zabibu Jumanne (8) aliyekuwa anasoma darasa la pili na Ramadhani Matatizo (12) aliyekuwa darasa la tano ilipatikana na kuzikwa Februari 25, siku moja tangu wazame maji wakati mwili wa Ashura Ramadhani (8) aliyekuwa anasoma darasa la kwanza ulipatikana na kuzikwa jana Februari, 28, mwaka huu.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu leo Jumatano Machi Mosi, 2023, Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kigoma, Jacob Chacha amesema mwili huo umepatikana Saa 8:00 mchana leo ukiwa unaelea juu ya maji pembezoni mwa kingo za Mto Luiche.

“Kuna uwezekano kuwa mwili wa mtoto Zabibu ulikuwa umebanwa na kitu chini ya maji na umeweza kutoka na kuelea juu ya maji kwa sababu ya ongezeko la wingi na kasi ya maji mtoni kutokana na mvua zinazonyesha,” amesema Kaimu Kamanda Chacha

Kaimu Kamanda Chacha amewashuruku wote waliojitolea kushiriki kwa hali na mali kufanikisha kazi ya uokoaji tangu ajali hiyo ilipotokea Februari 24, mwaka huu licha ya changamoto ya maji ya Mto Luiche kuwa wanyama wakali wakiwemo mamba na viboko.

Wanafunzi wanne waliopoteza maisha, wenzao wawili pamoja na nahodha wa mtumbwi waliokolewa walizama maji Saa 1:30 asubuhi ya Febaruari 24, 2023 baada ya mtumbwi wao kupinduka walipokuwa wanavuka Mtu Luiche kutoka mtaa wa Mgumile kwenda Shule ya Msingi Kagera.

Chanzo: Mwananchi
Related Articles: