Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jengo la maduka lateketea Shinyanga

Ew Moto Shy Jengo la maduka lateketea Shinyanga

Tue, 6 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mali za Wafanyabiashara wapatao 10 ambazo thamani yake bado haijajulikana, zimeteketea kwa moto ulitokea usiku wa kuamkia leo Juni 6, 2023 katika jengo la maduka linalomilikiwa na Umoja wa Wanawake Tanzania UWT mkoa wa Shinyanga, maarufu kama JJ, lilipo mkabala na ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA mkoa wa Shinyanga.

Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo, moto huo umeanza majira ya saa nane usiku na kusababisha vyumba saba vya maduka kuungua huku sita vikiokolewa.

Wakizungumza kwa masikitiko makubwa, baadhi ya wafanyabishara waliopoteza mali zao, wamesema walipigiwa simu usiku na mlinzi wakijulishwa kuhusu maduka yao kuteketea kwa moto, ambapo walitoa taarifa kwa Jeshi la zima moto na kufika kujaribu kuuzima moto huo, baada ya magari ya Jeshi hilo kuchelewa kufika katika eneo la tukio.

Akizungumzia tukio hilo Katibu wa UWT mkoa wa Shinyanga, Asha Kitandala, amesema tukio hilo limewarudhisha nyuma Wafanyabishara waliokuwa wakifanyia biashara katika jengo hilo na kwamba, UWT pia walikuwa wakilitegemea kwa mapato.

Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana, ingawa taarifa za awali zinaeleza kuwa,umetokana na hitilafu ya umeme. Juhudi za kulipata Jeshi la zimamoto kuzungumzia tukio hilo zinaendelea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: