Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dereva aliyesababisha vifo 18 akamatwa

ABWAO WEB Kamanda wa Polisi mkoani Tabora, ACP Richard Abwao.

Thu, 26 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi mkoani Tabora linamshikilia dereva wa lori la mafuta, Tallick Laufi, kwa madai ya kusababisha vifo vya watu 18 na kujeruhi 35 akiwamo dereva wa basi Dickson Rahimu, aliyevunjika viungo na kukazwa hospitali.

Kamanda wa Polisi mkoani Tabora, ACP Richard Abwao, alisema dereva wa lori alimsababishia kuvunjika viungo dereva wa basi katika tukio lililotokea Oktoba 21, maeneo ya Usongo, wilayani Nzega.

Ajali hiyo ilihusisha lori hilo lenye namba za usajili T 481 AGB ambalo lilikuwa likitokea jijini Dar es Salaam kwenda Mwanza na ilielezwa kuwa dereva wa lori alikuwa katika mwendo kasi akitaka kuyapita magari mengine ndipo alipoligonga basi hilo lenye namba T612 CQD lililokuwa likitolea jijini Mwanza kuelekea Dar es Salaam.

“Ajali hii imesababisha vifo vya watu 18 na kujeruhi 35 na kati yao 19 walipelekwa Hospitali ya Nkinga akiwamo dereva wa basi na wengine waliruhusiwa baada ya kupata matibabu, 15 bado wanaendelea kutibiwa,” alisema.

Abwao alisema, majeruhi wengine 31 walipelekwa Hospitali ya Wilaya Nzega, kati yao 26 waliruhusiwa na watano wanaendelea na matibabu, mmoja amepelekwa Hospitali ya Rufani Bugando Mwanza kwa uchunguzi zaidi.

Aliwataka madereva wa magari na wanaotumia vyombo vya moto kuchukua tahadhari wawapo barabarani na kuzingatia sheria zote husika ili kuepukana na ajali zinazopoteza maisha ya watu na mali zao na kuwasbabishia ulemavu wa maisha.

Uchunguzi wa gazeti ili imebaini kuwa basi hilo lilikuwa limepakia abiria zaidi ya 70 kupita kiwango kinachotakiwa kisheria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: