Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC ataka madarasa haya yabomolewe

MADARASA WE DC ataka madarasa haya yabomolewe

Tue, 7 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Mohamed Hassan Moyo ameamuru kuvunjwa kwa baadhi ya madarasa ya Shule ya Msingi Majogo katika Kijiji cha Litula Kata ya Marambo kutokana na uchakavu wa majengo ya Shule hiyo ambayo yanahatarisha maisha ya Wanafunzi na Walimu.

Akiwa katika ziara ya Kijiji kwa Kijiji yenye kauli mbiu isemayo "ulipo nipo toa kero yako sema kweli sio majungu", DC huyo amefanikiwa kufika katika Shule hiyo na kuikuta ikiwa katika hali ya uchakavu mkubwa wa majengo ambayo yanahatarisha maisha ya Wanafunzi na Walimu.

Moyo amesema haiwezekani Wanafunzi wakaendelea kusoma kwenye madarasa ambayo yamejawa na nyufa kila kona hivyo madarasa hayo yabomolewe haraka iwezekanavyo.

Amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea kujenga upya madarasa hayo ili Wanafunzi wa Kijiji cha Majogo waendelee kupata elimu inavyotakiwa kwa faida ya Taifa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: