Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bodaboda adaiwa kumjeruhi kwa mapanga mwanafunzi

PANGA Ed Bodaboda adaiwa kumjeruhi kwa mapanga mwanafunzi

Thu, 27 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Uduru wilayani Hai mkoani Kilimanjaro (jina tunalo) amecharangwa mapanga na dereva pikipiki (bodaboda) kwa tuhuma za kumpa simu mdogo wa bodaboda huyo iliyosababisha kutofanya vizuri katika masomo yake.

Mwanafunzi huyo alimweleza mwandishi wa habari hizi kuwa Julai 17 mwaka huu asubuhi, wakati anakwenda shuleni, alikutana na dereva huyo ambaye alichomoa panga na kuanza kumshambulia maeneo mbalimbali ya mwili ikiwamo kichwa, miguuni na mikononi.

"Ilikuwa asubuhi ninaelekea shuleni, nilikutana na bodaboda huyo, nikamsalimia hakuitikia. Ghafla alichomoa panga kiunoni na kuanza kunishambulia huku akinituhumu nimempa mdogo wake simu janja anayoitumia kuwasiliana na wanaume badala ya kusoma, jambo ambalo si kweli.

"Nilianza kupiga kelele katika kuomba msaada ndipo walipotokea wazee wawili wakaniokoa na baada ya hapo sikujua kilichoendelea hadi nilipojikuta nipo hospitalini daktari ananisafisha vidonda na kunifunga vitambaa vyeupe," alisema.

Baadhi ya mashuhuda, akiwamo Tumaini Tumsifu, walidai kuwa asubuhi siku hiyo, walisikia kelele za kuomba msaada ndipo walipotoka na kukutana na kijana huyo akiwa na panga lenye damu huku akitoa lugha za matusi.

Mwenyekiti wa kitongoji hicho lilikofanyika tukio hilo, Peter Masawe, alithibitisha binti huyo kutendwa ukatili huo na kijana huyo aliyemtaja ni Hilary Mafue, dereva bodaboda na alikimbizwa katika zahanati kupatiwa matibabu.

"Nilikwenda hadi zahanati ambako nilimkuta anapatiwa matibabu, kisha nikaenda polisi na kutoa taarifa tena. Kabla sijaenda niliwasiliana na mwenyekiti wa kijiji na kumpa taarifa, tukaongozana kwenda shuleni ambako tulikuta tayari wameshapata taarifa juu ya tukio.

"Bado ni tatizo kubwa kwenye matukio ya aina hii maana hata tunapochukua hatua ya kuwakamata na kuwapeleka kituoni baada ya muda wanaachiwa," alilalamika Masawe:

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: