Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Basi ya MOA latumbukia baharini Tanga

Basi Gari Baharini Qjalini WA0043 Basi ya MOA latumbukia baharini Tanga

Sun, 23 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Basi la Kampuni ya MOA linalofanya safari zake kutoka Tanga kupitia Pangani na kuvuka kwenye kivuko hadi Kipumbwi limezama wakati linatoka ndani ya kivuko cha MV Tanga ambacho kilikuwa kimefika mwisho wa safari eneo la feri ya Kipumbwi kikitokea Pangani.



Mkuu wa Wilaya ya Pangani Zainab Abdallah ambaye amefika eneo la tukio amesema hakuna aliyepoteza maisha wala Majeruhi kwenye ajali hiyo kwakuwa Abiria walikuwa wameshuka na kukaa ndani ya kivuko kama ilivyo kanuni za vivuko siku zote ambapo kwenye Basi alibaki Dereva pekee yake ambaye hata hivyo aliwahi kuruka wakati Basi lilipofeli breki na kutumbukia majini.

Kwa sasa juhudi za kulitoa gari hilo ndani ya maji zinaendelea kufanyika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: