Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba wa kambo ataka marehemu azikwe Kikristo na si Kiislam

Mwili Wazuiwa Muhimbili Baba wa kambo ataka marehemu azikwe Kikristo na si Kiislam

Wed, 21 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taharuki kubwa imeibuka huko Mkoani Mwanza baada ya mwili wa marehemu kufikishwa msikitini kuswaliwa kwa maziko lakini baba wa marehemu akazuia asizikwe.

Kwa mujibu wa maelezo ya mama wa marehemu huyo, kabla ya kuolewa mwanaume huyo alimkuta akiwa na mtoto wa miezi sita na kwamba mtoto huyo ana baba yake mwingine ambaye ni Mchaga na ni Muislamu.

Mara baada ya kufariki kwa mtoto huyo, mwanaume huyo ameibuka na kusema kwamba hataki mtoto huyo azikwe kiislamu huku mama wa mtoto akiweka wazi kwamba mtoto huyo siyo mkristo na hivyo anaomba mtoto wake azikwe kwa kufuata taratibu za dini yake ambayo ni dini ya kiislamu.

Aidha, kutokana na mvutano huo, Jeshi la Polisi limelazimika kuingilia kati na kuahirisha mazishi hayo mpaka pale mwanaume huyo aliyedai kwamba mtoto huyo asizikwe kiislamu ataporejea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: