Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba mbaroni kwa kumlawiti mtoto wake

Jela (1) Baba mbaroni kwa kumlawiti mtoto wake

Wed, 12 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Amani Martin mkazi wa kata ya Nzihi Halmashauri ya Wilaya ya Iringa anashikiliwa na Jeshi la Polisi tuhuma za kumlawiti mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa mwaka mmoja na kumsababishia maumivu makali.

Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Allan Bukumbi amesema mbinu aliyotumia mtuhumiwa ni kumshika mtoto kwa nguvu na kumfanyia kitendo hicho wakati wakiwa shambani baada ya mama wa mtoto kuondoka kwenda kuokota kuni na kumuacha mtoto akiwa na baba yake.

Kamanda Bukumbi amesema kiini cha tukio hilo bado kinachunguzwa na mtuhumiwa amekamatwa na taratibu za kisheria zinaendelea kuchukuliwa dhidi yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: