Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba adaiwa kumuua mkewe kisa wivu wa mapenzi

Mauaji Nn.jpeg Baba adaiwa kumuua mkewe kisa wivu wa mapenzi

Wed, 30 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la polisi mkoa wa PolisiTarime/Rorya linamshikilia Silasi Kokolo (50) kwa kuuawa kwa mke wake.

Kamanda mkoa wa Polisi Tarime/Rorya, Marco Njera amemwambia mwandishi wa gazeti hili kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa 2 asubuhi Agosti 29, 2023 akiwa njiani kwelekea Nyumbani kwao mtaa wa Kemoge halmashauri ya miji ya Tarime mkoani Mara.

"Jeshi la polisi linamshikilia kwa upelelezi Silasi Kokolo miaka (50) mkazi wa Kemoge kwa tuhuma za mauaji ya mke wake Furaha Silasi Kokolo miaka (47) kwa kumkata kata mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake na chazno cha tukio hilo ni wivu wa Mapenzi," alisema Kamanda Njera.

Kamanda huyo aliongeza kuwa upelelezi ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu mashitaka yanayo mkabili.

Kamanda Njera ametumia nafasi hiyo kuitaka jamii kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi badala yake wazingatie sheria wakati wanapokuwa wamehitilafiana kwenye ndoa.

Kwa upande wake Mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya inayomilikiwa na halmashauri ya mji wa Tarime, Yonam Charles alithibitisha kupokea mwili wa marehemu na kusema kuwa wamepokea mwili wa mwanamke ambaye amefariki dunia kwa kukatwa katwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake.

Tulipokea mwili wa mwanamke anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 30-40 Mnamo saa 4 asubuhi Agosti 29, 2023 ukiwa umekatwa katwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake na kusababisha kuvuja damu nyingi na kupelekea kifo chake na mwili wa marehemu upo chumba cha kuhifadhia maiti (MOCHWARI) ukisubiri maandalizi ya mazishi alisema Daktari huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: