Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baa 3 kati ya 31 zafunguliwa Mwanza

Baa 2 Recovered 0 Baa 3 kati ya 31 zafunguliwa Mwanza

Tue, 23 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Wila ya Ilemela Hassan Masala amewataka Wamiliki wa Baa na Hoteli Jijini Mwanza kuzingatia sheria na kanuni za undeshaji wa biashara zao kwani kukiuka kufanya hivyo na kuzalisha kelele sumbufu kutafanya waendelee kuchukuliwa hatua kali kwa mujibu wa taratibu za Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira ( NEMC).

Akiongea kwa niaba ya RC wa Mwanza, DC Masala amesema Uongozi wa Mkoa wa Mwanza kwa kushirikiana na NEMC Mei 5, 2023 walifanya kaguzi 50 kwa Wafanyabishara wa Hoteli na Baa na kubaini maeneo 31 ya biashara hizo kwenda kinyume na sheria hivyo kuchukuliwa hatua na kupewa maelekezo ya kudhibiti kelele sumbufu.

“Maeneo ya biashara yaliyobainika kukiuka sheria yametozwa faini ya Tsh milioni 2 huku waliotozwa milioni 5 wakiwa ni wale waliobainika kuwa sugu kwa kuzalisha kelele sumbufu licha ya kuonywa mara kadhaa na wametakiwa kuweka vifaa maalum vya kudhibiti kelele”

Jumla ya Baa 3 kati ya 31 za Mkoani Mwanza tayari zimekamilisha kulipa faini na kufuata miongozo ya NEMC hivyo wamepatiwa vibali vya kuendelea shuguli zao.

Itakumbukwa Mei 19, 2023 Wamiliki wa Baa na Hotel Jiini Mwanza walikutana kwa pamoja kujadili agizo la NEMC huku baadhi wakilalamikia kifaa cha kudhibiti sauti kuwa haikiendani na maelekezo ya NEMC na wengine wakitishia kusitisha kutoa huduma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: