Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Auawa kwa kuchomwa kisu kifuani

Kisu Mauaji Morogoro Auawa kwa kuchomwa kisu kifuani

Tue, 28 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Aubi Ndomi anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 38, Mkazi wa Mtaa wa Mji Mwema Kata ya Tungi Manispaa ya Morogoro, amefariki dunia mara baada ya kuchomwa na kisu kifuani na mtu ambaye jina lake bado halijajulikana, anayetajwa kuwa muuza nyama.

Global TV imefika hadi nyumbani kwa marehemu na kuzungumza na mama wa marehemu na mwenyekiti ambapo wamesema kuwa tukio hilo limetokea jana, Novemba 27, 2023 majira saa kumi jioni baada ya kutokea ugomvi kati ya marehemu na muuza nyama huyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo ambapo amesema kuwa jeshi hili linaendelea na uchunguzi wa kumsaka muuza nyama aliyetekeleza mauaji hayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: