Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Atupwa jela miaka 8 kwa kuua bila kukusudia

Sad Mauajis Atupwa jela miaka 8 kwa kuua bila kukusudia

Tue, 6 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama Kuu Kanda ya Tabora imemtia hatiani na kumuhukumu kutumikia kifungo cha miaka nane jela kwa kosa la mauaji ya bila kukusudia mwanamke mmoja anayefahamika kwa jina la Adela Haruna mkazi wa Kata ya Ipuli Manispaa ya Tabora.

Akisoma hukumu hiyo Jaji Mfawidhi wa mahakama hiyo, Athuman Matuma amesema mahakama imepitia hoja za pande zote mbili na kwamba Jamhuri imeweza kuthibitisha kuwa mshitakiwa, Adela alifanya mauaji hayo Machi 21, 2022 bila kukusudia baada ya kumpiga kichwani kwa fimbo kijana aliyefahamika kwa jina la Sadik Tito, hali iliyosababisha kifo chake baada ya kufikishwa hospitali.

Adella Haruna alikiri mbele ya mahakama hiyo kwa mara nyingine tena kutenda kosa hilo ambalo ni kinyume na kifungu cha 195 na 198 sura ya 16 kanuni ya adhabu iliyofanyiwa marejeo mwaka 2019.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: