Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Amfukia mkewe chumbani, mabaki ya marehemu yazua hofu

Mabaki Mauaji Amfukia mkewe chumbani, mabaki ya marehemu yazua hofu

Tue, 5 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Juma Peter mkazi wa Nyamhimbi wilayani Bariadi mkoani Simiyu, anatuhumiwa kumuua na kisha kumfukia mke wake ndani ya chumba walichokuwa wanalala na mara baada ya kufanya tukio hilo aliuza eneo hilo ambalo lilikuwa na nyumba ya tope na kuhamia sehemu nyingine.

Hali hiyo imebainika hii jana baada ya mtu aliyenunua eneo hilo kuanza shughuli za ujenzi ambapo jana wakati wachimbaji wakiendelea na zoezi la kuchimba msingi wakakutana na fuvu la kichwa cha binadamu.

Kwa mujibu wa mafundi hao wamesema wakati wakiendaelea na zoezi la ukamilisha wa uchimbaji wa msingi huo ambao walianza kuuchimba siku ya Jumamosi ndipo walipokutana na fuvu la kichwa cha mtu hatua iliyopelekea kutoa taarifa kwa fundi mkuu na fundi mkuu kumjulisha mtu mwenye kiwanja na mara baada ya mmiliki wa kiwanja kufika waliwaita viongozi wa mtaa ambao walilazimika kuwapigia simu polisi na mtuhumiwa kukamatwa.

“Leo (jana) tulikuwa kwenye hatua za mwisho kumalizia kuchimba msingi, ghafla tutakutana na fuvu la kichwa cha mtu, tulishtuka tukaamua kuwatafuta watu wa ngazi ya juu yetu tukawajulisha ili wajue. Hata kama mwanamke umemchoka bora ukamrudisha nyumbani kwao sio kumuua au kumfukia, hiki ni kitendo cha kinyama,” amesema mmoja wa mafundi.

Kwa upande Ofisa Afya wa Wilaya amesema; “Inaonekana ni mwanamke ambaye ana zaidi yam waka mmoja tangu amezikwa katika ardhi hii, hatujui kama aliugua au aliuawa, lakini lazima kama binadamu tuwe na utu, tusiwe na mioyo migumu mpaka kuzika wenzetu wakiwa wazima.”

Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa wa Nyamhimbi amesema mtuhumiwa alikuwa na tabia ya kuoa wanawake na kuacha huku Afisa Afya wa Halmashauri ya mji akithibitisha mwili huo kuwa wa mwanamke, ambao umezikwa kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Ofisa Tarafa wa Kata ya Ntuzu akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wialaya ya Bariadi; “Tulifika hapa tukauliza eneo hili ni la nani? Wakasema ni la Ofisa Mipango wa halmashauri ya Mjia ambaye aliuziwa na Juma.

“Tukamuita Juma tukafanya mahojiano naye kumuuliza mkewe anayeitwa Suzana yuko wapi? Akasema hajui alipo. Baada ya kumbana zaidi akasema ndiye ambaye alifariki na akamzika ndani ya nyumba yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: