Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Akutwa chumbani amefariki, wmili una siku 4

MAUAJIZ.png Akutwa amefariki

Sun, 13 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hassan Kanema (45) mkazi wa Amani Gongo Stoo Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja amekutwa akiwa amefariki dunia chumbani kwake Kwa siku nne bila ya kufahamika kuwa amefariki huku chanzo cha kifo chake kikiwa bado hakifahamiki hadi sasa.

Mwenyekiti wa Amani Gongo Stoo, Amani Maabadi amethibitisha "Wananchi tushirikiane usikubali kukaa pekee yako wakati unaishi na wenzio ili ukipata tatizo uwaaambie, kilichotokea ni kama maiti kanyimwa haki yake ya kusitiriwa maana Mtu akifariki lazima apate haki zake"

"Ana kawaida siku mbili tatu humuoni, siku hiyo tulikuwa tumegonga baada ya kupata wasiwasi kidogo, baadaye saa 4 akawa ameingia akiwa ameshika kiatu kimoja, tukamuuliza akasema kiatu kimoja nimekiacha ofisini Mtu akija ajue nipo, alipoingia hakutoka hadi tumekuja kukuta maiti" Mama mwenye nyumba, Bi Latifa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: