Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ajali iliyoua wanafunzi wawili Bahi, yajeruhi 31

Maitii Ajali iliyoua wanafunzi wawili Bahi, yajeruhi 31

Thu, 11 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanafunzi wawili wamefariki na majeruhi 31 wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma katika kituo cha afya cha Mpalanga wilayani Bahi.

Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Godwin Gondwe amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo katika kijiji cha Mpalanga wilayani Bahi huku akidai maiti za wanafunzi zipo mbili na majeruhi wapo 31.

Amesema majeruhi 13 wapo katika kituo cha afya cha Mpalanga huku wengine 18 wakilazwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

“Hii ni taarifa kamili wamefariki wanafunzi wawili na 13 wamelazwa katika kituo cha afya cha Mpalanga na wengine wapo hapa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma,” amesema Mkuu huyo wa Wilaya.

Mkuu huyo wa Wilaya amesema yupo katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma akihakikisha wajeruhi wanapatiwa matibabu yanayostahili.

Inadiwa wanafunzi hao walikuwa wakienda katika kijiji cha Maganga kwa ajili ya kushiriki michezo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: