Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahukumiwa kunyongwa kwa kumuua mnywaji mwenzake

Crime Scene 45.jpeg Ahukumiwa kunyongwa kwa kumuua mnywaji mwenzake

Tue, 20 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama Kuu Kanda ya Tabora imemhukumu Mwande Punguja (36), mkazi wa Kijiji cha Mwitungu, Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora, kunyongwa hadi kufa kwa kosa la kumuua Kagwa Alusha (35) kwa kumtumbukiza kisimani baada ya kutoka baa kunywa pombe.

Akisoma hukumu hiyo juzi, Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Tabora, Jovith Kato, aliyekasimishwa mamlaka ya jaji, alisema mshitakiwa alitenda kosa hilo Februari 6 mwaka huu katika Kijiji cha Mwitungu wilayani humo.

Alieleza kuwa wawili hao waliokuwa wakinywa pombe katika moja ya baa, waliondoka pamoja huku Alusha akiwa amebebwa kwenye baiskeli na Punguja.

Hakimu huyo alisema kuwa baada ya kufika eneo la kisima kirefu, Punguja aliamua kumdumbukiza kisimani na kumsababishia umauti kisha yeye kuendelea na shughuli zake bila kujali ukatili aliomtendea mwenzake.

Hakimu Kato alieleza kuwa kutokana na kosa hilo, mahakama hiyo ilimtia hatiani na kumhukumu kunyongwa hadi kufa kutokana na ukatili na kuondoa uhai wa mwenzake kwa makusudi.

Awali mshtaki alipohojiwa kuhusu mashtaka hayo, alikubali na kukiri kutenda kosa hilo la kumtumbukiza kisimani na kumsababishia kifo chake bila kujali kuwa mtu huyo alikuwa na familia inayomtegemea.

Akitoa ushahidi wake kuhusu tukio hilo, mmoja wa mashahidi wa upande wa Jamhuri, Kundi Ngelela ambaye walikuwa naye kwenye baa, alidai Alusha alibembwa na mshitakiwa kwenye baiskeli yake na kuondoka naye.

Shahidi huyo alisema kwamba alipofika nyumbani kwake, alitoka kwenda kwa Alusha hakumkuta ndipo alipoingiwa na wasiwasi. Wakaanza kumtafuta na wanafamilia sehemu mbalimbali bila mafanikio.

Alidai kuwa baadaye watu walisema kuna mtu katumbukia kisimani ndipo walipongozana na kuukuta mwili wake kisimani.

Katika kesi hiyo, Upande wa Jamhuri uliongozwa na Mawakili Alis Tomasi na Stev Mzava huku upande wa utetezi uliongozwa na Amosi Gahese.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: