Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afukua kaburi la mama yake na kukaa nalo ndani

Jenezaa Bg Afukua kaburi la mama yake na kukaa nalo ndani

Mon, 3 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanaume mwenye umri wa miaka 76 anayeitwa Marian L, nchini Poland anakabiliwa na kifungo cha kwenda jela baada ya kuchimba kaburi na kutoa mabaki ya mwili wa mamake na kuweka katika kochi lake, ukitazama televisheni, kwa miaka 13.

Mwanaume huyo mwenye huzuni, ambaye majirani zake hawakujua jina lake kwa sababu alikuwa “mtu mpweke,” alipigwa risasi mnamo Februari ndipo wakati shemeji yake alipomtembelea nyumbani kwake katika mji mdogo wa Radlin, ulio kusini magharibi mwa Poland na kukuta mwili huo sebuleni.

Shemeji yake alipogundua kuwa bwana Marian apigwa risasi aliwaita wahudumu wa afya; na walipofika, walikuta maiti iliyozimika ikiwa juu ya kochi, juu ya rundo la magazeti kutoka 2009.

Marcin Felsztyński, ambaye ni mkuu wa ofisi ya mwendesha mashtaka wa wilaya, alisema kuwa mwili huo ulikuwa “katika hali nzuri.” Felsztyński alieleza zaidi, “Kila kitu kinaonyesha kwamba mwanamume huyo alitumia baadhi ya kemikali kuhifadhi maiti.”

Afisa mwingine kutoka ofisi ya mwendesha mashtaka wa wilaya, Joanna Smorczewska, alisema, “Kulingana na matokeo ya DNA, maiti ni ya mwanamke, Jadwiga L aliyefariki Januari 2010, na ndiye mama yake na Marian L. ambapo alizikwa Januari 16, 2010, na walipochunguza wamekuta kaburi la Jadwiga L limebaki tupu.

Inaelekea bwana Marian aliufukua mwili wa mama huyo mara baada ya kuzikwa na kisha kubaki katika nyumba hii tangu 2010.” Inaarifiwa kuwa nyumba ya mwanamume huyo iko mita 300 tu kutoka kwenye makaburi ambayo mama yake alizikwa awali.

Sasa anakabiliwa na kifungo cha jela. Hivi majuzi alishtakiwa kwa kunajisi maiti, na mama yake anatarajiwa kuzikwa tena.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: