Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kinana ajiuzulu CCM

KINANA MAKAMBA NAPE Kinana ajiuzulu CCM

Tue, 30 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana amejiuzulu wadhifa huo baada ya kuomba mara kadhaa kwa Mwenyekiti wa CCM Taifa, Samia Suluhu Hassan ambaye sasa ameridhia ombi hilo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumatatu, Julai 29, 2024 na Katibu wa NEC ya CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makala imesema Kinana ameandika barua ya kuomba kupumzika.

Katika majibu yake Mwenyekiti wa CCM Samia amesema: "Ni kweli nilipokuomba utusaidie kwa nafasi ya makamu mwenyekiti nilikuahidi utakaa muda mfupi kama ulivyoomba, na kwa kweli nilipenda uendelee kutusaidia lakini kwa kuwa umeomba sana na ahadi ni deni nalazimika kwa moyo mzito kuridhia kujiuzulu kwako."

Rais Samia amesisitiza kuwa Chama kitaendelea kutumia uzoefu na maarifa ya Kinana kila itakapohitajika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: