Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dkt. Nchimbi: Magufuli ndiye aliyemtenegeza Samia

Samia Suluhu And President Magufuli Dkt. Nchimbi: Magufuli ndiye aliyemtenegeza Samia

Mon, 12 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amesema Hayati John Joseph Pombe Magufuli alimuamini na kumtengeneza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

"Pamoja na kazi nzuri ambazo Hayati Magufuli alizianzisha katika nchi yetu, ambazo zilitujengea heshima kubwa duniani, lakini pia Rais Magufuli ndiye alitutengenezea Rais wetu tuliyenae leo, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan," amesema Balozi Dkt. Nchimbi.

Katibu Mkuu huyo wa CCM amesema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi wa Chato, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Stendi ya Zamani, Chato mjini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: