Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania, Urusi kudumisha uhusiano

Nchimbi Urusi Tanzania, Urusi kudumisha uhusiano

Fri, 23 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi amesema kuwa CCM, chini ya Mwenyekiti wake Samia Suluhu Hassan itaendelea kudumisha uhusiano na urafiki wa muda mrefu kati ya Tanzania na Urusi, ukilenga kuboresha maeneo ya uwekezaji, biashara na uchumi, kwa ajili ya manufaa ya pande zote mbili.

Balozi Dk. Nchimbi amesema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Urusi nchini Tanzania, Andrey Avetisyan, ambapo amesisitiza kuwa kuboresha maeneo ya uwekezaji, biashara na uchumi, kutaimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya Serikali za nchi hizo mbili na wananchi wake na kuufanya kuwa wa moja kwa moja zaidi.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar es Salaam, pamoja na kurejea kumbukumbu za uhusiano wa muda mrefu wa Tanzania na Urusi, tangu wakati wa kupigania uhuru na baada ya uhuru, ambao mwaka huu unafikisha miaka 62, walizungumzia maeneo ambayo yanaweza kufanyiwa kazi na Serikali za nchi hizo, chini ya uongozi wa vyama vinavyoongoza nchi hizo, Chama Cha Mapinduzi na United Russia, mtawalia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: