Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Mbuzi washinda kesi ya uzururaji

Mbuzi Washinda.jpeg Mbuzi washinda kesi ya uzururaji

Tue, 25 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kundi kubwa la Mbuzi wakorofi wenyetabia ya kuzurura katikati ya mji kwa zaidi ya miaka 100 wameachiwa huru baada ya kushinda kesi ya uzururaji.

Baraza la Halmashauri ya Llandudno, North Wales iliamuru mbuzi hao kuwa huru licha ya tabia mbovu walizonazo wanyama hao za kula mimea na uzio wa nyumba za watu.

Kutokana na kusababisha maafa kwa jamii mara kadhaa wakazi wa Wales wamekuwa wakitaka kuwapiga risasi mbuzi hao ili watoweke kwenye makazi ya watu.

Mamla ya ya eneo hilo imeamua kuwa ni jukumu la wamiliki wa ardhi kulinda mali zao dhidi ya Mbuzi hao wazururaji badala ya kuzuiliwa.

Ripoti ya mwisho iliyotolewa na Baraza imewapa haki Mbuzi hao wa ‘Kashmir’ ikisema kwamba hawatawafungia wanyama hao ili wasizurure na badala yake wapo huru.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: