Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Mahusiano: Hakuna mume/mke wa mtu!

CHEAT HG Mahusiano: Hakuna mume/mke wa mtu!

Tue, 21 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wiki chache zilizopita, nilikuwa nyumbani kwetu kijijini Mkumbi, wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma. Ndiyo asili yetu, nilizaliwa kule, nimesomea kule hatua za awali na nzuri zaidi, ninajua kuzungumza lugha ya kwetu, KIMATENGO.

Wamatengo kiasili ni watu wakarimu na ni wengi jijini Dar es Salkaam na mikoa mingine. Uzuri mwingine pia juu yao, ni miongoni mwa makabila ambayo yamejitahidi kuwapeleka shule watoto wao, kiasi kwamba tunao ndugu zetu wengi tu katika nafasi mbalimbali kubwa serikalini, kwenye mashirika ya umma na hata taasisi binafsi.

Nikiwa hapa Dar ninao ndugu, jamaa na marafiki tunaotokea wote huko, kiasi ambacho tumeunda hadi umoja wa wamatengo. Sasa nikasafiri hadi kule, nikafika kijijini kwetu salama salimini.

Usiku wa saa mbili, simu yangu ikaingia ujumbe wa kunisalimia, nikaujibu na baadae ukaendelea kunijulia hali ya safari iliyosababisha niulize mwenzangu alikuwa ni nani.

Akajitambulisha. Asee, ni mmoja kati ya akina dada wamatengo ninayefahamiana naye tangu Dar, akinifahamisha kuwa yeye alikuwa Mbinga mjini na amepata taarifa kutoka kwa mmoja wa wanakijiji wenzangu juu ya ujio wangu. Nilifurahi sana.

Ni kitambo kidogo tulikuwa hatujaonana. Tulichat kwa muda mwingi, akinifahamisha kuwa alikuwa amehama jijini Dar na kuanzisha maisha Mbinga, akiwa ameolewa.

Baadaye, akanikaribisha kumtembelea hapo mjini, angalau tupate mbili tatu maana anajua mimi ni mtu wa bwax.

Kiutani, nikamwambia ninaogopa mwaliko huo kwa sababu yeye tayari ni mke wa mtu na kama waswahili wanavyosema, mke wa mtu sumu!

Huwezi kuamini, pengine naye kiutani akaniambia, hakuna kitu kama hicho duniani, hakuna mke wala mume wa mtu!

Of coz nilijua ni utani, ambao hata hivyo baadaye, nikaupa nafasi ya kuutafakari akilini mwangu. Tafakuri yangu ilitembea kufikia matukio mbalimbali tunayokutana nayo katika maisha yetu ya kila siku hasa kwa wanandoa, wenye uhusiano, wachumba na hata vijana wanaotafuta wenza wao wa kushare maisha!

To be honest, yule mdada alikuwa sahihi. Unabisha? Ninasimama naye kwa mifano kadhaa michache lakini yenye kufikirisha.

Kwanza, waswahili, tuna kawaida ya kupenda kujidanganya. Acha kudanganyana, ni kujidanganya, yaani wewe mwenyewe unajiapiza vitu vya uongo ili hali nafsi yako inafahamu kuwa ni uongo.

Tuanze kwako mwenyewe. Mimi nataka niamini kuwa wewe una umri unaoanzia miaka 18. Hebu iambie nafsi yako, uhusiano uliopo hivi sasa ni wa ngapi tangu uanze utundu?

Simaanishi kuwa wote ni waongo. La hasha, wapo wakweli, tena wakweli kabisa, lakini tukisema tuwakague, trust me, kama ile treni ya Kigoma imejaza watu kibao, wenye mtu mmoja katika maisha yao ya uhusiano, ni mmoja au wawili!

Nimeandika habari za udaku kwa miaka kadhaa. Katika mojawapo ya habari nilizowahi kukutana nazo, ni binti wa mchungaji kukutwa akiwa na ugonjwa wa ukimwi, baada ya jamii iliyomzunguka kuamini kuwa hakuwa mtundu. Siyo tu hakuonekana akiwa na mtu, lakini hata tabia zake zilishabihiana na dhana ya watu juu ya utakatifu wake. Na siyo kwamba aliupata ugonjwa huo kwa kurithi, no, kuna jibaba lilikuwa linatoka naye!

Maisha yetu ya uhusiano yanapitia maeneo mengi sana hadi tunapokuja kuamua kuoa au kuolewa. Huko nyuma, tunakuwa tumeacha watu wetu shule za msingi tulizosoma, sekondari, vyuo na pengine miji tuliyohama.

Unapokuja kukutana naye miaka kadhaa mbele, aina flan hivi ya dhambi ya asili inatukabili. Unaona kama vile si kitu kwa vile uliwahi kuwa naye labda au hata kama aliwahi kukutaka zamani mkiwa kwa mfano Singida, leo mmekutana Mtwara, unaona Why uendelee kumbania?

Lakini ukiacha hivyo, maisha yetu pia ya ndoa na uhusiano yana mazonge mengi. Kuna wanandoa hawaongei kwa sababu ya madhila mbalimbali. Baadhi hudhani kwa kushiriki tendo na mtu wa nje ni tiba!

Ndoa na uhusiano wetu pia imekuwa kama kichaka cha kuficha maovu yetu. Mtu atakuwa mkali na kusema yeye ni mke au mume wa mtu kwa mtu ambaye nafsi yake haimpendi, lakini pale anapokuwa dhaifu, ni rahisi, rahisi mno kuisaliti ndoa au uhusiano wake.

Ninawafahamu wake za watu wengi, wengine ni wake wa marafiki zangu, lakini wanashiriki mchezo huu mchafu. Mimi pia nina mke, na naamini wapo rafiki zangu wanamuona akifanya ndivyo sivyo. Wanaume ndiyo kabisaaaaaaa, hawafai hata kidogo.

Kwa kuwa wengi wetu tuna udhaifu huu wa kibinadamu, jambo la msingi kulikumbuka ni kutunza heshima, yako na ya mwenzio. Jitahidi kadiri unavyoweza kusaliti kwa staha. Nenda mbali na unapoishi, jitahidi kushiriki na mtu asiyemjua mwenza wako na cha msingi, TUMIA KINGA!

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: