Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watuhumiwa 150 wa mauaji wadakwa

3d117e3d497569b23f7fd92294cd00e4 Watuhumiwa 150 wa mauaji wadakwa

Tue, 1 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni ameunda kamati ili kushauri na kuja na mkakati wa kitaifa wa kukomesha mauaji.

Aidha alisema katika kipindi cha Januari Mosi mwaka jana hadi Januari 31 mwaka huu kulikuwa na matukio 176 na watuhumiwa 150 walikamatwa.

Masauni alitaja sababu kubwa za mauaji hayo kuwa ni kuwania mali, wivu wa mapenzi, visasi, ushirikina, migogoro ya ardhi, ulevi na kuchukua sheria mkononi

Aliwaeleza waandishi wa habari kuwa baada ya kufanya kikao na maofisa wa ngazi za juu ya jeshi hilo, ameamua kuunda kamati ya kuishauri serikali nini kifanyike ili kupata suluhisho la kudumu la mauaji.

Alisema kamati hiyo ambayo itatakiwa kutoa taarifa baada ya siku 21, itashirikisha wawakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani, Jeshi la Polisi, Ofisi ya Wakili wa Serikali, Usalama wa Taifa, na Ustawi wa Jamii.

Wawakilishi wengine ni kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na rushwa (TAKUKURU), Taasisi ya Elimu ya Juu, Ofisi ya Mwanasheria wa Serikali Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Alisema jopo hilo limepewa siku 21 kuja na mkakati wa Kitaifa wa kukomesha mauaji Nchini.

Alisema Serikali hailali usiku na mchana ili kuhakikisha matukio ya mauaji yanakomeshwa.

Alisema katika kikao hicho alipokea taarifa kuanzia Januari Mosi hadi Januari 31, katika maeneo Makuu mawili, Mosi,kuhakikisha matukio yanapotokea hatua za haraka zinachukuliwa ikiwemo watuhumiwa kuchukuliwa hatua za haraka.

Alisema katika kipindi hicho cha Januari Mosi hadi Januari 31 jumla ya matukio ya mauaji 176 yalitokea na mikoa vinara ni Kagera, Dodoma, Tabora, Mara, Kigoma na Songwe.

Pia aliwataka wananchi kujitokeza kutoa taarifa kwa kamati.

“Kuna Mzee mmoja analalamika sana kule Mtwara baada ya mtoto wake kuuawa, Serikali kukaa kimya jambo hilo litafanyiwa kazi.,” alisema.

Alisema wote wenye malalamiko kwenye matukio yaliyotokea waende kwenye vituo vya Polisi milango iko wazo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: