Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vijana vidole waliokatwa vidole na balozi wafunguka "Alitaka kutuua"

Vidoleee 651239 Vijana vidole waliokatwa vidole na balozi wafunguka

Mon, 11 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vijana wawili ambao ni ndugu wa familia moja Zephania Tinkson Mdolo (20) na Kelvin Tinkson Mdolo (17), wamedai kukatwa vidolegumba vya miguu na mtu aliyefahamika kuwa ni balozi wa nyumba kumi katika Kata ya Mpemba Mjini Tunduma mkoani Songwe kwa kuwatuhumu kuwa ni wezi.

Wakizungumzia tukio hilo lililotokea tarehe 03 Novemba vijana hao wanadai tarehe hiyo walikuwa kuchunga mifugo ndipo balozi aliwaita na kuwakata vidole na kuwabebesha Nondo akidai kuwa ni wezi wa Nondo.

Tulikuwa tunatoka kuchunga ng’ombe, balozi alituita akasema twendeni huku juu mkachukue vindoo vyenu, tulipofika kule akaanza kutupiga na kutukata vidole bila kosa lolote. Akatubebesha nondo na kuanza kusema sisi ni wezi.

“Balozi alisema tuwaue huku huku, lakini baba Alex akasema tuwakate vidole. Tulipofika nyumbani nikazirai, mdogo wangu alikuwa na nafuu kidogo, hatukuzungumza chochote. Tulibaki tumalala ndani tu,” wamesem vijana hao.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Songwe ACP Theopista Mallya amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema wanamshikilia Samwel Eckson Mnkondya, anayedaiwa kuwa ni balozi, kwa tuhuma za kuwakata vidole vijana hao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: