Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sele akamatwa tuhuma za kuwakata vichwa mama na mtoto

PANGA Ed Sele akamatwa tuhuma za kuwakata vichwa mama na mtoto

Mon, 27 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamke mmoja aitwaye Mwanaisha Matere (37) na Mtoto wake Baraka Maita mwenye umri wa miaka 7 Wakazi wa Kijiji cha Mavimba Kata ya Milola Wilayani Ulanga Mkoani Morogoro wameuawa kwa kuchinjwa shingo na kutenganishwa viwiliwili vyao na vichwa huku chanzo kikiwa bado hakifahamiki.

Diwani wa Kata ya Milola lilikotokea tukio hilo Masoud Mohamedi amesema kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Novemba 24, 2023 ambapo Majirani waliona damu zikichuruzika mlangoni na walipofungua mlango walikuta viwiliwili vya marehemu vikiwa havina vichwa.

Amesema katika nyumba hiyo walikuwa wakiishi na Mtu mmoja Mgeni ambaye alikaribishwa kama Mfanyakazi wa shamba lakini baada ya tukio hilo hakuonekana nyumbani hapo na wakati tukio linatokea baba wa familia hiyo alikuwa amesafiri na kuwaacha nyumbani hapo mke, Mtoto wake pamoja na Mgeni huyo ambaye anahisiwa kuwa ndiye aliyewaua na kuwakata vichwa Mama na Mtoto kisha kuondoka na vichwa.

Mkuu wa Wilaya ya Ulanga , Julius Ningu amethibisha kutokea kwa tukio hili ambapo amesema jitihada zinaendelea za kumsaka Mtuhumiwa wa tukio hilo.

Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro limesema baada ya msako mkali limefanikiwa kumkamata Selemani Sita (25) ambaye anadaiwa kumchinja Mama na Mwanae kwa kutenganisha vichwa na viwiliwili vya kuondoka na vichwa hivyo na kwenda kuvitupa Mtoni.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro, Alex Mkama amesema Sele alifika katika nyumba hiyo kwa lengo la kutafuta kazi ya kulima na aliishi kwa muda wa wiki mbili kisha kutekeleza tukio hilo.

RPC Mkama amesema baada ya kumkamata Selemani aliongozana na Polisi hadi alikotupa vichwa hivyo katika Mto Ulali uliopo katika Kijiji hicho ambapo kwa sasa upelelezi unaendelea na utakapokamilika atafikishwa Mahakamani ingawa RPC hajaweka wazi sababu ya Sele kuwachinja wawili hao na sababu ya kuvitupa vichwa hivyo Mtoni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: