Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi yanasa 11, ni wazee wa 'tuma hiyo pesa kwa namba hii'

Kamanda Mwaibambe Kamanda Mwaibambe.

Thu, 20 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi Mkoani Tanga wanawashikilia watu 11 wakiwahusisha na tuhuma za kutapeli watu fedha kupitia simu za mkononi.

Hayo yameelezwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga,Henri Mwaibambe wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kwamba watuhumiwa hao walikutwa na wakiwa na simu 11 za kuburuza na simu ndogo 13 pamoja na laini sa simu 399 ambazo zilikuwa zikitumiwa kwenye udanganyifu huo.

Kamanda Mwaibambe amesema watuhumiwa hao baada ya kufanyiwa upekuzi katika makazi yao walikutwa na vitu vingine ambavyo navyo ni pamoja na karatasi 43 za namba za mawakala zenye majina mbalimbali sambamba na vitambulisho mbalimbali 14 na pikipiki waliyokuwa wakiitumia kutekeleza malengo yao.

Alibainisha kuwa watuhumiwa hao ambao walikuwa wameweka kambi maeneo ya donge mkoani Tanga wanadaiwa kuendesha uhalifu katika mikoa mbalimbali hapa nchini na kuwaomba wananchi watoe ushirikiano na jeshi la polisi ili kuweza kukabiliana na wahalifu hao ili waweze kuchukuliwa sheria kali na tayari jeshi hilo limekwisha wafikisha mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria

Kamanda mwaibambe anasema baada ys kuwahoji kwa muda mrefu watuhumiwa hao walikiri njia walizokuwa wanazitumia kutapeli ambapo walikuwa wanawapigia watu au kutuma ujumbe mfupi (sms) kwa ajili ya kutumiwa pesa au kuomba namba za siri.

Katika tukio jingine polisi wanamshikilia Eliasi Yohana(27) mkazi wa Hambalawai wilayani Lushoto kwa tuhuma za kumuua Paulo Danieli ambaye alimuhusisha kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanamke ambaye anadai kuwa alikuwa na mahusiano naye.

Aidha, polisi wamesema wanawashikilia watu 105 kwa kuendesha pikipiki zenye makossa mbalimbali

Kamanda Mwaibambe amewataka watanzania kushirikiana na jeshi la polisi kukabiliana na vitendo vya kihalifu vinavyosababisha kuikosesha jamii Amani na kushiriki ipasavyo kwenye shughuli za kiuchumi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: