Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pili afikishwa mahakamani kwa mauaji

Lupita Nyongooo Z Pili afikishwa mahakamani kwa mauaji.

Wed, 10 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkazi wa Wilaya Nyamagana Jijini Mwanza Pili Selenge (47) amepandishwa kizimbani katika mahakama ya Wilaya ya Ilemela na kusomewa shtaka la mauaji.

Pili amesomewa shtaka hilo mnamo tarehe 09 January 2024 katika kesi ya jinai namba 640/2024 ambapo mshitakiwa anatuhumiwa kumuua mwanaume ambae bado jina lake halijafahamika kinyume cha kifungu namba 196 na 197 cha sheria ya kanuni ya adhabu Sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2022.

Akosomewa mashtaka hayo mbele ya Hakimu Fortunatus Kabuja ,mwendesha mashtaka wa Serikali Monica Mweli,amesema mshtakiwa alitenda kosa hilo Disemba 20,2023 katika eneo la Nyahonze Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza.

Baada ya kusomewa shtaka hilo, mshitakiwa hakutakiwa kijibu chochote kwa kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka kisheria kusikiliza kesi hiyo na shauri hilo limeghairishwa hadi Januari 22, 2024.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: