Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwenyekiti atupwa jela miaka 30 kwa kumbaka mtoto wa miaka 13

Jela Pic Data Mwenyekiti atupwa jela miaka 30 kwa kumbaka mtoto wa miaka 13

Thu, 13 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makama ya Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu, imemhukumu kifungo cha kwenda jela miaka 30 Mambo John (30) mkulima na mkazi wa kijiji cha Isengwa kwa kosa la kubaka.

John ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mwanginde ilidaiwa kuwa katika nyakati tofauti kati ya Mwezi January na May 2023 huko Kijiji cha Isengwa ndani ya wilaya Itilima alimbaka mtoto wa kike (jina linahifadhiwa) mwenye umri wa miaka 13 na kumsababishia ujauzito.

Kwa Mujibu wa mwendesha Mashtaka kutoka ofisi ya taifa ya mashtaka wilaya hiyo Mkaguzi msaidizi wa Polisi Jaston Mhule alielezea mahakama kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo kinyume na kinyume na kifungu cha 130(1)(2)e na 131(1) vya sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyo fanyiwa marejeo mwaka 2022.

Jumla ya mashahidi wanne na vielelezo viwili vilitolewa na upande wa mashtaka baada ya ushahidi huo mshtakiwa alijitetea mwenyewe na Makama kumkuta na hatia kwa kosa la kubaka.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo Roberth Kaanwa, Mwendesha Mashtaka aliomba Mshtakiwa apewe adhabu Kali ili iwe funzo kwake na kwa jamii ili wazee wenye umri kama yeye waache kuwarubuni watoto na kuwafanyia vitendo hivyo.

Mshtakiwa aliomba mahakama impunguzie adhabu kwani ni mkosaji wa mara ya kwanza na anafamilia inamtegemea, na ndipo Hakimu akamhukumu kifungo cha miaka 30 jela na fidia ya Sh. 500,000 kwa mhanga.

Katika hatua nyingine Mahakama hiyo pia imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela Emmanuel Kuyi mkazi wa kijiji cha Mwamapalala Wilayani humo kwa kosa la kumbaka mtoto wa kike (8).

Kabla ya hukumu iliyotolewa na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo Roberth Kaanwa, Mwendesha Mashtaka kutoka ofisi ya taifa ya mashtaka wilaya hiyo Mkaguzi msaidizi wa Polisi Jaston Mhule alielezea mahakama kuwa Mshitakiwa akiwa ni baba mlezi wa mtoto huyo mnamo tarehe 5/5/2023 majira ya mchana huko Kijiji cha mwamapalala ndani ya Wilaya Itilima alimbaka.

Mshtakiwa aliomba mahakama impunguzie adhabu kwani ni mkosaji wa mara ya kwanza na anafamilia inamtegemea, ndipo Hakimu alipomhuku kifungo cha miaka 30 jela.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: