Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mume mbaroni kwa tuhuma za mauaji ya mkewe

Gereza Ajabu Pingu Mume mbaroni kwa tuhuma za mauaji ya mkewe

Mon, 10 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara linatarajia kumfikisha mahakamani Kizito Odilo Achula (42), mkazi wa Ligula C, Manispaa ya Mtwara Mikindani kwa tuhuma za mauaji ya mke, Victoria Almas (41).

Akizungumza na waandishi wa habari jana Jumapili, Aprili 9, 2023, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Nicodemus Katembo alisema siku ya tukio usiku wa Aprili 7, 2023 Achula aliingia ndani na kufunga mlango kisha kuanza kumpiga mkewe.

Kwa mujibu wa kamanda huyo mtuhumiwa huyo alikuwa akimpiga mkewe mateke maeneo mbalimbali ya mwili ikiwemo tumboni, kifuani na usoni, shambulio ambalo lilisababisha kukatisha uhai wa mwanamke huyo.

Alisema uchunguzi wa awali umebaini mtuhumiwa alikuwa na tabia ya kumpiga mkewe mara kwa mara hivyo wamekuwa na ugomvi wa muda mrefu.

“Mpaka sasa upelelezi wa tukio hilo umekamilika na muda mfupi ujao mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma za mauaji,” alisema Katembo

Alitumia fursa hiyo kutoa rai kwa wananchi wa mkoa wa Mtwara kuacha kujichukulia sheria mkononi kama kuna mgogoro ndani ya familia ni vyema migogoro hiyo ikatatuliwa kwa njia ya amani sio kujichukulia sheria mkononi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: