Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto auawa, atolewa sehemu za siri

Faa84aafd42c4b428b01344233e57519.jpeg Mtoto auawa, atolewa sehemu za siri

Wed, 2 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu wasiojulikana wamemuua mwanafunzi wa darasa la nne katika Shule ya Msingi Tutuo, wilayani Sokonge, Mkoa wa Tabora, Maria Ngassa (13) na kunyofoa sehemu zake za siri.

Mtoto huyo alikuwa akiishi katika Kitongoji cha Ulula, Kijiji cha Muungano, Kata ya Tutuo na aliuawa wakati akienda kisimani kuchota maji.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa polisi wanachunguza kubaini chanzo cha mauaji hayo na wauaji waliohusika.

Baba wa mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina la Ngassa Kazungu alisema mwanawe aliuawa Januari 29, mwaka huu.

Alieleza kuwa, siku ya tukio Maria alirudi nyumbani saa 11:00 jioni akitoka shuleni na mama wa mtoto huyo alimtuma akachote maji kisimani.

Alisema Maria alikwenda kuchota maji na kurudi nyumbani, lakini alipokwenda kwa mara ya pili hakurudi na mwili wake uliokotwa kichakani siku iliyofuata ukiwa umenyofolewa sehemu ya siri na pia masikio yametobolewa na kitu chenye ncha kali.

"Jamani wananchi mwenzenu nimepata pigo kubwa sana ambalo sitalisahau katika maisha yangu, mtoto wangu Maria ameuawa kikatili sana, niliamua kumsomesha mwanangu ili siku za mbeleni aje kunisaidia lakini wameamua kukatiza maisha yake laah, naumia sana," alisema Kazungu huku akilia.

Mkuu wa Wilaya ya Sikonge, John Palingo alisema amepata taarifa kuhusu tukio hilo lakini alikuwa jijini Dar es Salaam kwa matibabu.

Mwenyekiti wa Serikali Kitongoji cha Ulula, Masele Charles alisema mtoto huyo aliuawa katika Kitongoji cha Ulula.

Diwani wa Kata ya Tutuo, Rashid Magope alisema mauaji hayo yanaleta taswira mbaya kwenye kata hiyo kwani mwaka jana kuna mwanafunzi wa sekondari aliuawa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: