Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mdogo wa marehemu asimulia A-Z alichokishuhudia kwa macho yake Swalha akiuawa

Mdogo Wa Swalher Swalha na mumewe

Mon, 30 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Imekuwa ni simanzi kwa familia ya Swalha kufuatia tukio la mauaji ya mwanamke huyo ambaye alikuwa akijishughulisha na masuala ya urembo (make-up artist) kuuawa na mumewe aliyetambulika kwa jina la Said linazidi kuibua mambo mengi na mzito.

Usiku wa kuamkia jana Jumapili Mei 29, 2022 Swalha alidaiwa kuuawa na Said kwa kupigwa risasi 7 za kichwani nyumbani kwao, Buswelu jijini Mwanza. Taarifa kutoka kutoka kwa watu wa karibu zinasema kuwa chanzo ni wivu wa kimapenzi.

Yapo madai ambayo yamekanushwa na ndugu wa marehemu kwamba Said alimkataza Swalha asiende kwenye shoo ya msanii Diamond Platnumz, lakini akakaidi na kwenda huko.

Jamaa huyo inasemekana naye alitishia kwenda kujiua na kutokomea kusikojulikana. Hata hivyo, mdogo wa marehemu ambaye walikuwa pamoja nyumbani wakati wa tukio, amesimulia A-Z alichokishuhudia wakati wa tukio la dada yake kuuawa na mumewe.

Mama wa marehemu anasimulia; “Watoto wangu (akiwemo Swalha) waliitwa na baba yao hapa nyumbani (Mei 28, 2022), walipofika baba yao akapata dharura hivyo hakuzungumza nao nikabaki nao tukawa tunataniana tu.

"Wakati tukio linatokea ilikuwa majira ya saa 2 kasoro, nilikuwa jikoni ghafla nikasikia milio ya risasi, nikasimama karibu na mlango wa chumbani kwao, nikaita dada, shemeji, kimya, nikarudi jikoni, baadae nikasikia tena risasi inapigwa nikarudi mlangoni nikaita, nikaona kimya, nikaenda tena jikoni.

"Mwenzangu (mama wa jirani) niliyekuwa naye akaniambia tuondoke, nikasema siwezi kumuacha dada yangu ana matatizo. Kwa sababu mara ya kwanza ilipopigwa nilisikia dada akipiga kelele, ndipo ikapigwa tena nyingine, akapiga tena mpaka risasi nne.

"Sisi tulisikia risasi nne, lakini tulivyoenda chumbani tulikuta maganda ya risasi yalikuwa saba, na nyingine zilipita mpaka kwenye ukuta.

"Kwenda nilisikia mlango unafunguliwa, ambapo ndipo shemeji alitoka, nikaingia chumbani nikamkuta dada yangu anamwaga damu nyingi, nikakimbia kwenda kuomba msaada kwa majirani.

"Ugomvi wa mara ya kwanza ulipotokea majirani walikatazwa kukanyaga pale, shemeji akasema hao ndio wanaosababisha, kwa hiyo majirani ikawa ngumu kuja nyumbani.

"Ikabidi niende mpaka Mbogamboga kutafuta bodaboda waje kunisaidia, wakaja wawili lakini wakakataa kuingia chumbani kuchukua mwili wakihofia itakuwa kesi nyingine. Mimi na mwenzangu tukaingia chumbani tukamtoa dada mpaka sebureni.

"Wale bodaboda wakawapigia simu polisi, wakaja askari wawili na bodaboda. Askari mmoja ndiye akachukua gari akaanza kuendesha tukampeleka mpaka Hospitali ya Bugando. Tuliporudi nyumbani tukamkuta baba ameshafika, akaongea na askari wakamueleza kilichotokea.

"Polisi walivyoingia chumbani kuchunguza walikuta simu mbili, moja ya mtuhumiwa (alikuwa na simu mbili, moja aliacha na nyingine akaondoka nayo). Simu nyingine ilikuwa ni ya dada ambayo baada ya kupekua walikuwa alikuwa akirekodi ugomvi wote, askari wakaichukua wakasema kisifutwe kitu.

"Walipiga picha za marehemu, wakachukua simu wakaondoka nayo pamoja na yale maganda ya risasi, wakafunga mlango wakasema usifunguliwe wala tusifute hizo damu," amesema mdogo wa marehemu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: