Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbaroni kwa kuiba nguo za ndani za wanawake

Chupi Dg Mbaroni kwa kuiba nguo za ndani za wanawake

Tue, 25 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Joel Kimurgor (19) anashikiliwa kwa kuiba nguo za ndani (chupi) za Wanawake katika Kijiji cha #Tegeyat, Kaunti ya Nandi, kufuatia mfululizo wa kutoweka kwa ajabu kwa nguo hizo zilizoripotiwa katika eneo hilo.

Kwa wiki kadhaa, kumekuwa na visa vya Wanawake kuripoti upotevu wa nguo zao za ndani kutoka kwenye kamba nyakati za usiku ambapo walianzisha zoezi la upekuzi kutoka nyumba moja hadi nyingine ndani ya kijiji hicho.

Siku ya Jumatatu, Aprili 23, 2023, Kijana huyo alipatikana na chupi hizo ndani ya nyumba yake na alikiri kuiba ili kumfurahisha mpenzi wake ambaye alimwomba amnunulie nguo mpya za ndani kama njia ya kuonyesha mapenzi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: