Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kitanzi chamng’ang’ania aliyeua, kupora Sh1 milioni

Kulawitiss Kitanzi chamng’ang’ania aliyeua, kupora Sh1 milioni

Tue, 13 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Rufani Tanzania imebariki adhabu ya kunyongwa hadi kufa aliyopewa mkazi wa Kijiji cha Kibubwa Wilaya ya Butiama mkoani Mara, Waryoba Elias, aliyehukumiwa kwa kumuua Chacha Isenye kwa panga na kupora Sh1 milioni.

Jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufani limetupilia mbali sababu moja ya rufaa aliyoiwasilisha, kuwa Mahakama Kuu Musoma ilimtia hatiani kwa kuegemea ushahidi dhaifu wa utambuzi wa mke wa marehemu, Wankuru Chacha.

Maelezo ya kosa lililosababisha ahukumiwe kifo yanaeleza kuwa usiku wa Novemba 1, 2017, marehemu Isenye akiwa amelala na mkewe, kundi la watu lilivamia nyumbani kwake na na mbwa wakaanza kubweka.

Isenye aliamka kwenda kuangalia kwa nini mbwa wanabweka mfululizo, ndipo alivamiwa na watu wenye mapanga na rungu, ambao walimkatakata maeneo mbalimbali ya mwili.

Isenye alipaza sauti akimwambia mkewe anakufa, ndipo mkewe alipoamua kwenda nje kumuokoa mumewe, lakini alikutana na kundi la watu watano wenye mapanga na marungu waliomuamuru arudi ndani.

Alidai kuwa Elias aliyekuwa miongoni mwa watu hao, alimlazimisha Wankuru arudi ndani na awape fedha, ndipo kwa kutumia tochi walizokuwa nazo walimulika chumba chote kutafuta fedha na Wankuru aliwapa Sh1 milioni.

Kwa mujibu wa ushahidi huo, Wankuru alimtambua mrufani kwa kuwa anaishi jirani na nyumba yao na kuwa baada ya kupora, watu hao walifunga mlango kwa nje ili asimuokoe mumewe.

Hata hivyo, anasema alifanikiwa kutoka kupitia dirishani na kwenda kuomba msaada kwa majirani na walipofika walimkuta mumewe amenyanyuka na kufanikiwa kuingia ndani. Baadaye walimpeleka Isenye Kospitali ya Bugando, ambako alifariki dunia.

Mabishano ya kisheria

Wakati wa usikilizaji wa rufaa hiyo, Wakili Edson Philipo aliyekuwa akimtetea mrufani, alisema aliishangaa Mahakama Kuu Musoma kwa kumtia hatiani na kumhukumu kifo mteja wake kwa kuamini mwanga wa tochi uliomulikwa chumbani.

Wakili huyo alijenga hoja kuwa kama watu walioingia katika nyumba ya marehemu, walimulika mwanga wa tochi kuelekea kwa Wankuru, ingekuwa vigumu kwake kumuona na kumtambua mrufani katika mazingira hayo.

Hata hivyo, jopo la mawakili wa Serikali, Tawabu Issa, Isihaka Mohamed na Agma Haule, walisema mashtaka dhidi ya mrufani yalithibitishwa kwa kuegemea ushahidi wa mke wa marehemu, ambaye ushahidi wake ulikuwa wa kuaminika.

Mawakili hao walisema mrufani alitambuliwa vizuri kutokana na mwanga uliokuwa ukitoka katika tochi mbili, umbali kati ya mrufani na mke wa marehemu ilikuwa ni hatua tatu tu na mrufani alikuwa ni mtu anayejulikana kwa familia hiyo.

Halikadhalika, walisema mara tu baada ya tukio hilo, mke wa marehemu alimtaja mrufani kuwa miongoni mwa watu waliowavamia, hivyo kutoa hakikisho la ubora wa ushahidi wake na kuondoa shaka kuwa atakuwa amemchanganya.

Hukumu ya rufani

Baada ya kuchambua hoja za mawakili wa pande zote mbili, jopo la majaji watatu wa mahakama ya rufani, Rehema Mkuye, Lugano Mwandambo na Issa Maige, walitupilia mbali hoja za wakili Philipo na kutupilia mbali rufaa hiyo.

“Baada ya kuupitia ushahidi ulioko kwenye kumbukumbu za mahakama, ni wazi kuwa mwanga wa taa uliomwezesha shahidi wa kwanza (Wankuru) kuwatambua majambazi ulitokana na mwanga wa tochi uliomulika chumba chote,” walisema katika hukumu yao ambayo ilipatikana jana katika mtandao wa mahakama kuu wa Tanzil.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: