Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Binamu aliyemng'oa mtoto macho atupwa jela miaka 40 jela

Mtoto Sagini Binamu aliyemng'oa mtoto macho atupwa jela miaka 40 jela

Tue, 25 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya mjini Kisii imewapata watu watatu na hatia ya kumng’oa mtoto Sagini macho, tukio lililofanyika mwaka jana na kuwashangaza watu wengi ndani ya nje ya Kenya.

Watatu hao ni pamoja na binamu wa mtoto Sagini Alex Maina Ochogo, shangazi yake Pacifica Nyakerario na bibi yake Rael Mayaka.

Mahakama hiyo katika kesi ambayo imekuwa ikifuatiliwa kwa miezi kadhaa iliwapata wote wakiwa na hatia ya kumng’oa mtoto Sagini macho na kuwhukumu vifungu tofauti tofuati kulingana na ushahidi uliotolewa kuwahusisha na kitendo hicho cha kinyama.

Binamu Alex Ochogo mwenye umri wa miaka 27 alihukumiwa kifungo cha miaka 40 jela kwa kuhusika moja kwa moja katika kutekeleza kitendo hicho.

Shangazi Nyakerario alihukumiwa miaka 10 jela huku bibi Mayaka akihukumiwa kifungo cha miaka 5 jela mtawalia.

Mahakama ilisema kwamba kifungo hicho kiliambatanishwa na ushahidi uliowasilishwa mahakamani lakini pia kigezo cha umri wao wa sasa.

Shangazi Nyakerario ana miaka 51 huku bibi Rael Mayaka akiwa na miaka 80.

“Mahakama inaangazia wajibu ulioshikiliwa na kila mmoja wa wakosaji katika kumng’oa mtoto macho. Mtoto alipoteza macho mikononi mwa binamu yake Alex Ochogo, akiwa kama mshtakiwa wa kwanza hapa. Nimeshindwa kubaini kupunguziwa kwake hatia kwa njia yoyote,” alisema jaji Ogweno.

Mahakama iiwapata shangazi na bibi kama waliosaidia kufanikisha kitendo hicho na mchano wao uliwatia hatiani vile vile.

Kabla ya tukio hilo la Desemba mwaka jana, mahakama ilibaini kwamba mtoto Sagini alikuwa anaishi maisha yenye siha njema pasi na ulemavu wowote mwilini akiwa chini ya malezi ya bibi yake Rael Mayaka.

Hata hivyo, Hakimu Ogweni alisema kuwa tukio hilo la Desemba 13 mwaka 2022 lilileta mabadiliko hasi katika maisha ya mtoto Sagini kabisa kwani alipoteza macho yake na kutangazwa kuwa kipofu kabisa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: