Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aua na kunyofoa moyo wa marehemu, aupika kisha kulisha familia yake

Moyo Mauaji Fgd Aua na kunyofoa moyo wa marehemu, aupika kisha kulisha familia yake

Wed, 29 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Lawrence Paul Anderson mwenye umri wa miaka 44 alifanya mauaji hayo mwaka wa 2021, chini ya mwezi mmoja baada ya kuachiliwa mapema kutoka gerezani.

Mwanaume huyo wiki kadhaa baada ya kuachiliwa, alifanya mauaji na kuuchomoa moyo wa Andrea Blankenship, kisha akaupeleka kwenye nyumba ya shangazi na mjomba wake na akapika moyo huo na viazi. Kulingana na shirika la habari la NBC

Kama ilivyo ripotiwa hapo awali, alijaribu kuwaandalia chakula wanandoa hao (shangazi na mjomba wake)kabla ya kufanya mauaji tena  ya kuwachoma Leon Pye mwenye umri wa miaka 67 na mjukuu wake wa kike Kaeos Yates mwenye umri wa miaka 4.

Lawrence Paul Anderson, 42, alikiri makosa matatu siku ya jumatano  ya mauaji ya kiwango cha kwanza na shtaka moja la shambulio la silaha.

“aliingia nyumbani kwa kutumia bega lake kuvunja mlango wa nyuma,”

“alimuua mwanamke mweupe nyumbani kwake na kuuondoa moyo wake kisha akapika moyo nyumbani kwa Pye na kujaribu kuwafanya Delsie na Leon Pye kula moyo kabla ya kuwashambulia.”

Hati ya kiapo ya pili inadai kwamba Anderson aliwaambia polisi kwamba alipika moyo huo na viazi “ili kulisha familia yake ili kuwatolea mapepo,” gazeti la Oklahoman liliripoti.

Anderson alihukumiwa kifungo cha maisha jela bila msamaha kama sehemu ya makubaliano ya maombi huko katika jimbo la Oklahoma nchini Marekani.

Mwendesha mashtaka alitupilia mbali mipango ya hukumu ya kifo kufuatia ombi kutoka kwa familia ya mwathiriwa.

Baada ya hukumu hiyo, mwendesha mashtaka, Jason Hicks, alisema katika mkutano na waandishi wa habari kwamba familia ya mwathiriwa haikutaka kuvumilia uchungu wa kesi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: