Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askari wanaotuhumiwa kumuua George Floyd wakutwa na hatia

MGN 1280x960 00604P00 UOIKW 1024x768 Askari wanaotuhumiwa kumuua George Floyd wakutwa na hatia

Sat, 26 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama nchini Marekani hatimae imewakuta maafisa watatu wa polisi wa zamani wa Minneapolis na hatia ya kukiuka haki za kiraia za George Floyd. Tou Thao, J. Alexander Kueng, na Thomas Lane walishtakiwa kwa kumnyima Floyd haki yake ya matibabu wakati Afisa Derek Chauvin alipomkandamiza kwa goti shingoni George Floyd kwa zaidi ya dakika tisa alipokuwa amefungwa pingu barabarani mnamo Mei 25, 2020.

Polisi hao Thao na Lane pia walishtakiwa kwa kukosa kuingilia kati kumzuia Chauvin katika Mauaji hayo ambapo Kueng alipiga magoti kwenye mgongo wa Floyd, Lane alishikilia miguu yake na Thao akawazuia waliokuwa karibu.

Chauvin alipatikana na hatia ya mauaji mwaka jana katika mahakama ya serikali na kuhukumiwa miaka 22.5.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: