Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyemchoma moto mkewe hadi kufa huku akimrekodi naye anyongwa

Tang Lu.jpeg Lamu na Tang Lu

Sat, 23 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Unyama wa kutisha! Hivyo ndivyo unavyoweza kusema kufuatia mwanaume mmoja nchini China qmbaye amenyongwa leo baada ya kukutwa na hatia latika kesi iliyokuwa ikimkabili ya kumchoma Mke wake moto hadi kufa huku akimrekodi video kupitia mtandao wa TikTok.

Tang Lu alimchoma moto mke wake wa zamani Septemba 2020, huku akirekodi moja kwa moja tukio hilo la kikatili jambo lililopelekea mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 30 kufariki wiki kadhaa baadaye wakati akitibiwa kutokana na majeraha makubwa aliyoyapata.

Mahakama katika eneo hilo imetoa taarifa yake fupi siku ya leo kwamba imetekeleza hukumu hiyo ya kifo cha Tang Lu japokuwa Tang alikuwa amekata rufaa dhidi ya hukumu yake ya kifo lakini akashindwa Januari mwaka huu.

Kesi hiyo iliyozua shutuma nyingi na hasira nchini China kutokana na matukio ya kikatili wanayokumbana nayo Wanawake katika ndoa zao.

Dada wa Lamu alivieleza vyombo vya habari vya Shangai kuwa ndugu yake alikuwa akipata manyanyaso makali na vipigo vya mara kwa mara kutoka kwa mumewe huyo, hali iliyosababisha waachane.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: