Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyejaribu kuwatoroka polisi afariki dunia kwa kupigwa risasi

Marco G Chilya Marco G Chilya.

Wed, 5 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma limesema limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa moja na mwingine kuuawa ambapo walikuwa wakijihusisha na uvunjaji maduka na nyumba kwa kutoboa paa na kufanya wizi.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi (SACP) Marco G Chilya amesema, mnamo tarehe 4.06.2024 majira ya saa sita usiku Maeneo ya Ruhuwiko Stendi walipata taarifa kuwa kutafanyika uhalifu wa uvunjaji maduka ndipo wakafanikiwa kuwakamata waalifu.

Chilya amesema mtuhumiwa mmoja alimtaja mwenzake anayeshirikiana naye ni Francis Ngonyani Severianus na wakamfuatilia na mkumkamata lakini alipopelekwa kwenye gari na kumwona mwenzake akaanza kukumbia, jambo ambalo lilipelekea polisi kumpiga risasi ya Mguu na kusababisha kuvuja damu nyingi, hivyo kupoteza maisha akiwa amekimbizwa Hosptalini.

Awali wafanya biashara wa Manispaa ya Songea walilamikia watuhumiwa hao kuvunjiwa maduka 22 na kuibiwa na jeshi la polisi kufanikiwa kuwakamata wezi sita,hivyo kuendelea na msako na kufanikiwa kuwakamata wengine wawili huku Mmoja akifariki.

Aidha, Chilya amesema mtuhumiwa huyu ambaye ni Marahemu alifika Manispaa ya Songea Tar 02.04.2024 akitokea jijini Dodoma ambako alikimbia baada ya mshirika mwenzake aitwaye Japhet Nyoni kuuawa kutokana na matukio ya uvunjaji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: